MAKALA YANGU
WANAWAKE WANAOFANYA BIASHARA YA KUUZA
MIILI YAO KWA WANAWAKE WENZAO NCHINI TANZANIA
Na
LILIAN JOSEPH NYINGISYE-0657583558.
Katika siku za
hivi karibuni tumeshuhudia wimbi kubwa la wasichana kwa wanawake nchini Tanzania wakijiingiza katika mapenzi
ya jinsia moja (usagaji). Jambo ambalo limeshika hatamu kwa sasa katika miji
mingi kama Dar es salaam,Arusha, Mwanza
na miji mingine mikubwa hapa nchini.
Japo hili jambo
lilikuwepo tangu zamani (kwasababu nakumbuka nilipokuwa mdogo nilipata
kushuhudia wasichana wawili wanandugu wa rika moja wakichapwa kwa shutuma za
kushiriki mapenzi ya jinsia moja) na hilo nimepata kuligundua sasa hivi nikiwa
na akili za kutambua mambo kwamba wale wasichana walikuwa ni wasagaji baada
yakukumbuka maneno waliokuwa wanaambiwa”hamuoni aibu kutembea wasichana watupu”
Kwa kipindi hiki
chote mambo haya yalikuwa yanafanyika kwa siri na wahusika walikuwa
wanajitahidi wasigundulike wala kuhisiwa kwamba wanajihusisha na mambo hayo.
kwasababu ilikuwa ikigundulika unaonekana ni mtu usiye na maadili,kwa familia
na jamii yote na unaweza kutengwa na wasagaji
walikuwa wanaona aibu kugundulika kuwa
ni wa aina hiyo.
Kwa hivi sasa mambo
yamebadilika sana jambo hili limekuwa si
siri tena,watu wanalifanya kuwa jambo la kawaida,walipo wanataka wajulikane
wapo si mitaani wala kwenye sherehe watu hawa hawana uwoga na vitu
wanavyofanya. Imefikia wakati hadi wanaongelea maswala ya kuwa na haki zao na
kutambulika kama makundi mengine yanavyotambulika(Tunashukuru bado hatujafikia
huko na serikali imesimama kidete kwa kupiga vita na kukemea vikali mahusiano ya kimapenzi ya jinsia moja)
Lakini tatizo
hili linazidi kuwa kubwa na sasa usagaji umekuwa si starehe tu bali ni
biashara,biashara kama zilivyo biashara zingine za halali maana zimekuwa na maeneo rasmi kabisa yanayojulikana
kama kwenye kumbi kubwa za starehe zilizo jijini,maeneo ya magomeni ambapo kuna
sehemu maarufu sana kwa shughuli hizo na kupata huduma hizo.
Na kuna watu wapo wanaishi mjini kwa kutegemea
biashara ya kuwa uza wasichana hao na kuwanunulia wateja wale wanao wahitaji.
Na wengine hutegemea biashara hii kuendesha maisha yao.”nilpokuwa sekondari nilikuwa
nafanya kama starehe tu lakini sasa hivi hii ndio kazi inayoniweka mjini”
anasema muathirika wa usagaji
Wasichana wanaojihusisha na mapenzi na
biashara ya aina hii wamekuwa na mbinu
mbalimbali za kuhakikisa biashara yao inatambulika na jamii kwa kuanzisha mitandao yao ya kijamii kama blogu na kurasaza facebook mfano wasagaji
na wasagaji crew hii ni mitandao
inayotumika kunadi nakutangaza biashara yao ya mapenzi ya jinsia moja.
Sasa hatuna budi
kujua ni nini kinachowasibu wanawake hawa ambao ni dada,mama,rafiki ,jirani na
ndugu zetu wajiingize katika mahusiano ya namna hii, Kwa muda mrefu sasa kuna watu wanaamini usagaji au tabia za
kisagaji ni za kuzaliwa (sababu za kibaolojia) japo wanasayansi na madaktari wenyewe wameshindwa kuthibitisha
hilo moja kwa moja kwa maana tafiti
nyingi zilizofanywa zimeshindwa kuthibitisha hivyo”tafiti hazioneshi moja kwa moja
kwamba tatizo la mahusiano ya jinsia mojani ya kibaolojia” A.Dean Byrd
2001.
Lakini muda
mwingine tabia hii inatokana na kuiga pamoja
na kushawishiana baina ya waichana wenyewe.Wasichana wanaigana na
kufundishana wanapokuwa pamoja na kwa
muda mrefu kama kwenye shule za bweni,vyuoni, marafiki walioshibana au kwenyekambi.pia kuangalia katika filamu za
ngono na mitandao mbalimbali “mimi nilianza kushiriki hii kama biashara
baada ya siku moja kuangalia filamu na nilipomuhadithia rafiki yangu ambae nae
yuko kama mimi tuliafikiana na kuamua kuanza”.anasema muathirika wa usagaji
Utandawazi na sayansi
na teknolojia vimekuwa vinatumiwa vibaya sana na vijana wa kitanzania (tofauti na kusudi la waliovumbua teknolojia
hiyo) kwakuiga vitu vingi hasi wanavyoviona kwenye mitandao bilakupima na
kuangalia athari zake.
Vilevile makundi
yameonekana ni kichocheo kikubwa yanayoharibu wasichana wengi kwa kushauriana
vitu ambavyo hawana uhakika navyo kwani
wasichana wengi wanafikiria kusagana ndio suluhisho la matatizo ya
mahusiano ya kimapenzi na mwanaume na kufanya biashara hii pia huwa ni ushauri
kutoka kwenye makundi hayo ( sio mara
zote) .
Wasichana wengine
wamekua wakifanya biashara hii kwaajili
ya tamaa ya vitu vizuri nawasivyo na uwezo navyo(hii ni kutokana na mashindano
yaliyopo ya kushindana vitu kama simu,magari,pesa,kwenda sehemu za gharama na
kuvaa vizuri), vitu ambavyo wasichana wengi kwasasa wana pigana ili kuvimiliki.
Hivyo kujikuta wakiingia ama kwa ridhaa zao au
kuingizwa na marafiki zao ili waweze kuwa juu hapa mjini kama wanavyosema
wenyewe,ndio maana kwenye hii biashara kuna wasichana tofauti kuanzia wanafunzi
wa sekondari,vyuo, wake za watu na hata wasanii wakubwa wenye majina yao hapa nchini ‘katika hii biashara kila mtu
ananunuliwa muda wmingine mwanaume( anaesaga) analipwakumtimizia mtu mahitaji
au mwanamke(anaesagwa )analipwa kumtimizia mtu mahitaji yake” anasema muathirika wa usagaji
Pia kuna tatizo
la umaskini na ugumu wa maisha unaoshamiri kila siku unawafanya wasichana
kukata tamaa na kutafuta njia za mkato na haraka kutafuta namna ya kujikimu
kimaisha bila kungalia nn athari zake nimewahi kukutana na msichana mdogo wa miaka 17(wakati huo 2009) alikubali kuishi
kinyumba na msichana mwenzie kwasababu tu mwenzie alikuwa akimkidhia mahitaji yake.
Pia wapo
wanaotolewa vijijini kwa minajili ya kuja kutafutiwa ama kufanya kazi kwenye
miji mikubwa lakini wakifika huku vibao vinawabadilikia na kukuta wameingia katika mikono ya manyang,au
yenye tamaa na kuijua miji na kuwaingiza kwenyebiashara hizo za mapenzi ya
jinsia moja.
Kwa vyovyote
vile malezi pia ni jambo
linalochangia sana wasichana
kuharibika na kujiingiza katika makundi
haya ya kibazazi,watoto wengi
sikuhizi hasa sehemu za mjini wanajilea wenyewe au kwa uangalizi mdogo wa
majirani,( uangalizi ambao si salama wakati mwingine) kwasababu wazazi wengi
wapo kukimbizana na maisha ambayo yanakimbia kwa kasi sana ivyo kuacha watoto
wanajiongoza wenyewe na kukutana na
madhira ya kuingizwa au kufundishwa michezo hii na watu wanaowazunguka.
Pia malezi mengine
ni yale tunayoyaita ya kizungu ( malezi ya kumwachia mtoto uhuru kupita kiasi
bila kufwatilia nyendo zake ),yanachangia kuumiza kizazi hiki tulichonacho kwasababu
watoto wanajikuta wanaiga na kuishi mambo ambayo hayafai na hawayaelewi ivo
kuishia kutenda kile wanachokiona kwenye televisheni na mitandao na sherehe wanazojumuika pamoja na
wazungu wenzao wa kiafrika (ambazo mara nyingi sherehe hizo hutawaliwa na
uzungu mwingi).
Mbali na hayo
mmomonyoko wa maadili katika jamii umeonekana ni kikwazo sana kufanya ili jambo lisiishe ama kupungua,.maana
swala hili la wasichana kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja linashindwa
kupigiwa kelele maana hadi watu wazima wapo katika biashara hii,sasa kunakuwa
hakuna wa kumkanya mwenzie (watatoa mifano ipi hao wakubwa watakaowakanya wadogo
wakati wakubwa wenzao wanayafanya hayo mambo tena wengine hadharani),
kwa kuwa watu
wengi wakubwa kwa wadogo wamekuwa hawaheshimiani wadogo wanatembea na wakubwa,
wakubwa wanatembea na wadogo hadi wameleta na misemo yakuhalalisha mambo yao “mtoto wa mwenzio ni mkubwa
mwenzio”.
Vyombo vya
habari na matukio yake wanayoyaonesha na kuandika yanahamasisha vitu kama
hivi(utakuta gazeti limeandika ahongwa gari na anaesagana nae, hivyo wasichana
wengine wataiga kwakuwa wanajua kuna faida) ,japo kuna sababu ya kuonesha umma
kilichotokea lakini wanatoa au kuonesha picha ambazo zinahamasisha na kuchochea
hili jambo na ivyo watoto na vijana wengi kukuta wanaiga na kuyatenda yale yanaoneshwa.
Wasichana
kutokua na elimu sahihi kuhusu mahusiano ya jinsia moja,kwa kuwa wasichana
wengi hujifunza tabia hizi kutoka kwa marafiki zao ambao huwahadithia na
kuwaelezea vitu kwa kuvipamba au wanapoangalia kwenye filamu na huwa
vimeongezewa nakshi ili kuwavutia wanaotazama na hivyo dada zetu ,rafiki zetu
na ndugu zetu hujikuta wameingia kwenye biashara hiyo kwa kutaka kuona jinsi
watakavyofaidika na mapenzi hayo.
Mitazamo pia
inawafanya watu kujiingiza katia hii biashara kwa kuwa wasichana wengi
waliojiingiza katika maahusiano haya uona,mahusiano haya yana raha zaidi
kushinda ya kushirki na mwanaume.kwa kuwa wameshaweka mitazamo hiyo huona kweli
na kuendeleza misimamo yao ambayo inaendelea kuwapoteza wengine wana msemo wao
”wanaume
pasua kichwa” hivyo mahusiano
hayo yana nafuu.
Kwenye wengi
kuna mengi na ukistaajabu ya Musa utayaona ya firauni, kuna wengine wanaofanya
mahusiano haya ni fasheni na ndio kwenda na wakati na kujua utandawazi,wanaona
sifa kuitwa au kuonekana wasagaji hasa watu maarufu kama wanamuziki na
waigizaji.
Sawa
tumelifumbia macho jambo hili na kufanya kama hatulioni hata tukiliona hashtuki
na tukishtuka tunashtuka kidogo nakuacha maisha yaendelee,tunalionea aibu
kulizungumza nakulijadili kwenye kadamnasi kwakuogopa kuonekana tunatetea au
tunashabikia vitendo hivyo.
Lakini kiukweli
imefika wakati tuongee na jamii na familia kueleza watoto wetu, dada zetu, mama
zetu na rafiki zetu kwamba kitendo hiki
cha mahusiano ya jinsia moja yanaathari nyingi katika jamii na wanaojihusisha
na mahusiano hayo.
Maradhi ni
hatari moja kubwa iliyopo katika mahusiano ya jinsia moja, maradhi kama
magonjwa ya zinaa (kaswende na,kisonono),mambukizi ya virusi vya UKIMWI na
uwezekano wa kupata kansa ya shingo ya kizazi kutokana na mfumo mzima na vifaa
wanavyotumia wakati wa kujamiiana ambavyo vina ruhusu majimaji ya miili yao kukutana na hivyo
kuwawekakatika hatari kama mmoja ameathirika”Maambukizi yapo ya magonjwa ya
zinaa,UKIMWI na hata ri ya kupata kansa ya shingo ya kizazi kutokana na
majimaji na vifaa” AlisemaDr. Merdad Paschal Nyalali kutoka Haydom Lutheran Referal Hospital Manyara.
Pia wanawake
wengi wanaojihusisha na biashara hii hujihusisha kimapenzi na watu wengine
wanawake kwa wanaume hivyo kuwa katika mapenzi ya mtandao ambayo ni hatari kwa
maambukizi ya magonjwa mbalimbali”Baaadhi ya watu naoshirikiana nao wana
boifrendi(wapenzi )wao nawengine ni wake
za watu”. Anasema muathirika wa usagaji.
Matatizo ya
kisaikolojia pia huwakumba wanawake wengi wanaoingia katika mahusiano haya
,japo wana sababu zao mbalimbali,za kujiingiza katika biashara hii lakini
mioyoni mwao wanajua kwamba jambo hili si jema na halikubaliki kwenye
jamii kwahiyo huwa hawajiamini na huona
kama wanaonewa(ndio maana mara nyingi watu wa namna hii huwa na maneno machafu
na matusi).
Wasagaji wale wanaosaga wenzao huwa wanajihisi
niwanaume na huwa hawataki kuitwa au kufananishwa na wanawake,huvaa, hutembea
na kuwa na tabia kama za kiume.
Mara nyingi
wasagaji huwa ni watumiaji wazuri wa madawa ya kulevya na vileo ili kuweza
kuhimili misongo waliyonayo”marafiki zangu hutumia vitu vikali ili
kupata stimu unajua hii kazi saa zingine haiendi bila hivo vitu…mimi huwa na
tumia pombe tu kawaida”.
Watu wenye
mahusiano ya kimapenzi ya jinsia moja
wanapojulikana ni nadra sana kupata nafasi za kuajiriwa kwakuwa
wanaonekana watofauti katika jamii na hamna mtu anaekubali kampuni au taasisi
yake iwe na watu wa aina hiyo kwa kuwa hata eleweka katika jamii.
Kidini pia, dini
zote hazikubaliani na vitendo hivi,hivyo mara nyingi kunatokea kutokuelewana
kunapotokea kashfa kama hizi sehemu za ibada. Pia ni rahisi sana kwa watu wa
aina hii kutengwa na kutokuruhusiwa kuingia nyumba za ibada kama misikitini na
makanisani.
Usagaji huchochea Mmomonyoko wa maadili kwa
kuwa watu wengi wanakua hawaheshimiani
na kwavile mambo haya yanafanywa hadharani hadi watoto wadogo wanaonana kudharau
na wengine na hivyo kuipelekea jamii kuwa ndivyo sivyo.
Mimi naamini kwa
kushirikiana kwetu kama wananchi na wanajamii tunaweza kulishinda hili tatizo
kwa kufanya na kuwajibika yafuatayo.
Sheria zipewe meno zaidi na ztumike ipasavyo
kudhibiti vitendo hivyo,kwasasa Tanzania inayo sheria inayokataza mahusiano ya
jinsia moja “Sheria ya makosa ya jinai 2002 kifungu 157 inakataza mahusiano ya
kimapenzi ya jinsia moja na adhabu yake ni miaka mitano” lakini sheria
hii inaonekana kulegalega na watu waliowengi hawaijui na hivyo kutofanya kazi
ipasavyo.
Hivyo basi kuna
kila sababu ya kuanza kuzifwatilia hizi sheria nakuhakikisha zinafanya kazi
ipasavyo nakuisaidia jamii na nchi yetu kwa ujumla.
Itolewe elimu ya
kina kwa wasichana hawa kuwaeleza madhara ya biashara wanayofanya kiafya kwamba
kuna uwezekano mkubwa wa kupata magonjwa
ya zinaa na ukimwi.Na waache kujidanganya kwamba hayo mapenzi ni salama.
Viongozi wa dini
watusaidie katika hili kukumbusha waumini wao nini dini haitaki kuhusu mapenzi
haya ya jinsia moja. Elimu na mafunzo ya
kidini pia yatolewe kwenye ngazi ya familia ili kuweka misingi imara na iliyo
bora kwa watoto.kila mzazi hakikishe kwamba anamfundisha na kumtia hofu ya
Mungu mtoto wake.
Wazazi
wahakikishe wanapata muda wa kufatilia
mienendo ya watoto wao wanapokuwa,wanaposhinda,michezo wanayocheza na watu
wanaoshi nda nao.Wawajengee uhuru na uwezo wa kusema na kueleza yale
yanayowasibu (maana watoto wengi katika familia za sasa hivi hawana zile nafasi
za kueleza matatizo na mambo yanayowasibu).Hivyo kukuta watoto wanatendewa vitu visivyofaa lakini
hawawezi kusema na wazazi wanapokuja kushtuka mtoto keshaharibika.
Maeneo hatarishi
yafutwe na kuondelewa mfano zile sehemu maarufu
kama nyumba zawahaya (samahani lakini ndivyo zinavyoitwa) maeneo mbalimbali
jijini Dar es salaam yaondolewe maana yanachochea na kufundisha watoto tabia
zisizofaa.
Vilevile
zitungwe sheria kulinda na kuongoza sehemu hizi za starehe,maana vitendo hivi
vinafanyika na tunajua vinafanyika lakini sheria haiwabani wenye kumbi hizi,sasa
sheria zikija na kuwabana hili tatizo litapungua na kuisha kabisa.
Jambo jingine
litakaloweza kuweka mambo sawa katika tatizo hili ni kuwekwe mifumo mizuri ya
kiuchumi itakayomwezesha mwanachi wa kada mbalimbali kuweza kupata fursa sawa
ya kumiliki mali,na kuweza kukidhi mahitaji yake ya kilasiku na familia yake.
Nikinukuu maneno
kutoka kwenye makala inayosema”USHOGA NI MATUNDA YA
MIFUMO MIBAYA YA KIUCHUMI NA JAMII” ya aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha Waandishi
wa Habari Wanawake(TAMWA) Bi Ananilea Nkya anasema”ushoga na usagaji ni moja ya
matunda mabaya ya mfumo wa uchumi wa kibepari ambao kwa kawaida hutoa fursa kwa
wachache wenye nguvu za kimadaraka na kifedha na kuwaacha wananchi wengi wakiwa
wamechanganyikiwa kutokana na kukosa fursa ya kupata ujira na maisha endelevu”hivyo
basi kuna haja ya kuurekebisha mfumo uliopo ili uweze kuwa mfumo wenye kutoa
fursa kwa watu wote na hivyo kupunguza watu wakiwemo wasagaji kutafuta njia za
mkato za maisha.
Kizuri zaidi huu
mfumo utawezesha watu kutotumia muda mwingi kuzunguka katika kutafuta riziki
kwa kuwa fursa zitakuwa za wote. Na hivyo kutumia muda mwingi na watoto na
familia na kujua maendeleo yao na
mienendo yao kwa ujumla.
Tuzingatie na
kufwata maadili yetu yaliyopo tufundishe jamii yetu kuhusu utandawazi katika
mlengo chanya na si kama ilivyosasa ambapo kila mtu hadi watoto wanajifunza
wenyewe na marafiki zao kuhusu mitandao na kompyuta. Na vyombo vya habari
vizingatie maadili yaliyopo hata kama yapo kibiashara zaidi.
Na serikali
kupitai mamlaka ya mawasiliano (TCRA) ingetafuta namna ya kudhibiti baadhi ya
programu ambazo hazina manufaa kwa wananchi na taifa kwa ujumla (kama walivyo
fanya China )
Hili ni tatizo,
hatuna budi kulikubali na kulifanyia kazi kama wanajamii ifike mahali
tulijadili hili swala kwa uwazi na ukweli na kutengeneza jamii isiyo na
mahusiano ya kimapenzi ya aina hii.kwa maana ukweli tunaujua na hatuna budi
kuukabili pia tatizo lipo hatuna budi kulitatua
maana wanasema dawa ya tatizo ni kulitatua si kuikimbia.
HII MAKALA NILIANDIKA NILIPOKUWA NAJIFUNZA KUANDIKA MAKALA