Monday, October 24, 2016

MAKALA YANGU



WANAWAKE WANAOFANYA BIASHARA YA KUUZA MIILI YAO KWA WANAWAKE WENZAO NCHINI TANZANIA
 Na LILIAN JOSEPH NYINGISYE-0657583558.
Katika siku za hivi karibuni tumeshuhudia wimbi kubwa la wasichana kwa wanawake  nchini Tanzania wakijiingiza katika mapenzi ya jinsia moja (usagaji). Jambo ambalo limeshika hatamu kwa sasa katika miji mingi  kama Dar es salaam,Arusha, Mwanza na miji mingine mikubwa hapa nchini.
Japo hili jambo lilikuwepo tangu zamani (kwasababu nakumbuka nilipokuwa mdogo nilipata kushuhudia wasichana wawili wanandugu wa rika moja wakichapwa kwa shutuma za kushiriki mapenzi ya jinsia moja) na hilo nimepata kuligundua sasa hivi nikiwa na akili za kutambua mambo kwamba wale wasichana walikuwa ni wasagaji baada yakukumbuka maneno waliokuwa wanaambiwa”hamuoni aibu kutembea  wasichana watupu”
Kwa kipindi hiki chote mambo haya yalikuwa yanafanyika kwa siri na wahusika walikuwa wanajitahidi wasigundulike wala kuhisiwa kwamba wanajihusisha na mambo hayo. kwasababu ilikuwa ikigundulika unaonekana ni mtu usiye na maadili,kwa familia na  jamii yote na unaweza kutengwa na wasagaji  walikuwa wanaona aibu kugundulika kuwa ni wa aina hiyo.
Kwa hivi sasa mambo yamebadilika sana  jambo hili limekuwa si siri tena,watu wanalifanya kuwa jambo la kawaida,walipo wanataka wajulikane wapo si mitaani wala kwenye sherehe watu hawa hawana uwoga na vitu wanavyofanya. Imefikia wakati hadi wanaongelea maswala ya kuwa na haki zao na kutambulika kama makundi mengine yanavyotambulika(Tunashukuru bado hatujafikia huko na serikali imesimama kidete kwa kupiga vita na kukemea vikali  mahusiano ya kimapenzi ya jinsia moja)
Lakini tatizo hili linazidi kuwa kubwa na sasa usagaji umekuwa si starehe tu bali ni biashara,biashara kama zilivyo biashara zingine za halali maana  zimekuwa na maeneo rasmi kabisa yanayojulikana kama kwenye kumbi kubwa za starehe zilizo jijini,maeneo ya magomeni ambapo kuna sehemu maarufu sana kwa shughuli hizo na kupata huduma hizo.
Na kuna  watu wapo wanaishi mjini kwa kutegemea biashara ya kuwa uza wasichana hao na kuwanunulia wateja wale wanao wahitaji. Na wengine hutegemea biashara hii kuendesha maisha yao.”nilpokuwa sekondari nilikuwa nafanya kama starehe tu lakini sasa hivi hii ndio kazi inayoniweka mjini anasema muathirika  wa usagaji
 Wasichana wanaojihusisha na mapenzi na biashara ya aina hii wamekuwa  na mbinu mbalimbali za kuhakikisa biashara yao inatambulika na jamii kwa kuanzisha  mitandao yao ya kijamii  kama blogu na kurasaza facebook mfano wasagaji na wasagaji crew  hii ni mitandao inayotumika kunadi nakutangaza biashara yao  ya mapenzi ya jinsia moja. 
Sasa hatuna budi kujua ni nini kinachowasibu wanawake hawa ambao ni dada,mama,rafiki ,jirani na ndugu zetu wajiingize katika mahusiano ya namna hii, Kwa muda mrefu sasa  kuna watu wanaamini usagaji au tabia za kisagaji ni za kuzaliwa (sababu za kibaolojia) japo  wanasayansi na madaktari wenyewe wameshindwa kuthibitisha hilo moja kwa moja  kwa maana tafiti nyingi zilizofanywa zimeshindwa kuthibitisha hivyo”tafiti hazioneshi moja kwa moja kwamba tatizo la mahusiano ya jinsia mojani ya kibaolojia” A.Dean Byrd 2001.
Lakini muda mwingine  tabia hii inatokana na kuiga pamoja na kushawishiana baina ya waichana wenyewe.Wasichana wanaigana na kufundishana  wanapokuwa pamoja na kwa muda mrefu kama kwenye shule za bweni,vyuoni, marafiki walioshibana au  kwenyekambi.pia kuangalia katika filamu za ngono na mitandao mbalimbali mimi nilianza kushiriki hii kama biashara baada ya siku moja kuangalia filamu na nilipomuhadithia rafiki yangu ambae nae yuko kama mimi tuliafikiana na kuamua kuanza”.anasema muathirika wa usagaji
Utandawazi na sayansi na teknolojia vimekuwa vinatumiwa vibaya sana na vijana wa kitanzania  (tofauti na kusudi la waliovumbua teknolojia hiyo) kwakuiga vitu vingi hasi wanavyoviona kwenye mitandao bilakupima na kuangalia athari zake.
Vilevile makundi yameonekana  ni kichocheo kikubwa  yanayoharibu wasichana wengi kwa kushauriana vitu ambavyo hawana uhakika navyo kwani  wasichana wengi wanafikiria kusagana ndio suluhisho la matatizo ya mahusiano ya kimapenzi na mwanaume na kufanya biashara hii pia huwa ni ushauri kutoka kwenye  makundi hayo ( sio mara zote) .
Wasichana wengine  wamekua wakifanya biashara hii kwaajili ya tamaa ya vitu vizuri nawasivyo na uwezo navyo(hii ni kutokana na mashindano yaliyopo ya kushindana vitu kama simu,magari,pesa,kwenda sehemu za gharama na kuvaa vizuri), vitu ambavyo wasichana wengi kwasasa wana pigana ili kuvimiliki.
 Hivyo kujikuta wakiingia ama kwa ridhaa zao au kuingizwa na marafiki zao ili waweze kuwa juu hapa mjini kama wanavyosema wenyewe,ndio maana kwenye hii biashara kuna wasichana tofauti kuanzia wanafunzi wa sekondari,vyuo, wake za watu na hata wasanii wakubwa wenye majina yao hapa nchinikatika hii biashara kila mtu ananunuliwa muda wmingine mwanaume( anaesaga) analipwakumtimizia mtu mahitaji au mwanamke(anaesagwa )analipwa kumtimizia mtu mahitaji yakeanasema muathirika wa usagaji
Pia kuna tatizo la umaskini na ugumu wa maisha unaoshamiri kila siku unawafanya wasichana kukata tamaa na kutafuta njia za mkato na haraka kutafuta namna ya kujikimu kimaisha bila kungalia nn athari zake nimewahi kukutana na  msichana mdogo wa  miaka 17(wakati huo 2009) alikubali kuishi kinyumba na msichana mwenzie kwasababu  tu mwenzie alikuwa akimkidhia mahitaji yake.
Pia wapo wanaotolewa vijijini kwa minajili ya kuja kutafutiwa ama kufanya kazi kwenye miji mikubwa lakini wakifika huku vibao vinawabadilikia na kukuta  wameingia katika mikono ya manyang,au yenye tamaa na kuijua miji na kuwaingiza kwenyebiashara hizo za mapenzi ya jinsia moja.
Kwa vyovyote vile malezi pia ni  jambo linalochangia  sana wasichana kuharibika  na kujiingiza katika makundi haya ya  kibazazi,watoto wengi sikuhizi hasa sehemu za mjini wanajilea wenyewe au kwa uangalizi mdogo wa majirani,( uangalizi ambao si salama wakati mwingine) kwasababu wazazi wengi wapo kukimbizana na maisha ambayo yanakimbia kwa kasi sana ivyo kuacha watoto wanajiongoza wenyewe na  kukutana na madhira ya kuingizwa au kufundishwa  michezo hii na watu wanaowazunguka.
Pia malezi mengine ni yale tunayoyaita ya kizungu ( malezi ya kumwachia mtoto uhuru kupita kiasi bila kufwatilia nyendo zake ),yanachangia kuumiza kizazi hiki tulichonacho kwasababu watoto wanajikuta wanaiga na kuishi mambo ambayo hayafai na hawayaelewi ivo kuishia kutenda kile wanachokiona kwenye televisheni  na  mitandao na sherehe wanazojumuika pamoja na wazungu wenzao wa kiafrika (ambazo mara nyingi sherehe hizo hutawaliwa na uzungu mwingi).
Mbali na hayo mmomonyoko wa maadili katika jamii umeonekana ni kikwazo  sana kufanya ili jambo lisiishe ama kupungua,.maana swala hili la wasichana kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja linashindwa kupigiwa kelele maana hadi watu wazima wapo katika biashara hii,sasa kunakuwa hakuna wa kumkanya mwenzie (watatoa mifano ipi hao wakubwa watakaowakanya wadogo wakati wakubwa wenzao wanayafanya hayo mambo tena wengine hadharani),
kwa kuwa watu wengi wakubwa kwa wadogo wamekuwa hawaheshimiani wadogo wanatembea na wakubwa, wakubwa wanatembea na wadogo hadi wameleta na misemo yakuhalalisha  mambo yao “mtoto wa mwenzio ni mkubwa mwenzio”.
Vyombo vya habari na matukio yake wanayoyaonesha na kuandika yanahamasisha vitu kama hivi(utakuta gazeti limeandika ahongwa gari na anaesagana nae, hivyo wasichana wengine wataiga kwakuwa wanajua kuna faida) ,japo kuna sababu ya kuonesha umma kilichotokea lakini wanatoa au kuonesha picha ambazo zinahamasisha na kuchochea hili jambo na ivyo watoto na vijana wengi kukuta wanaiga  na kuyatenda yale yanaoneshwa.
Wasichana kutokua na elimu sahihi kuhusu mahusiano ya jinsia moja,kwa kuwa wasichana wengi hujifunza tabia hizi kutoka kwa marafiki zao ambao huwahadithia na kuwaelezea vitu kwa kuvipamba au wanapoangalia kwenye filamu na huwa vimeongezewa nakshi ili kuwavutia wanaotazama na hivyo dada zetu ,rafiki zetu na ndugu zetu hujikuta wameingia kwenye biashara hiyo kwa kutaka kuona jinsi watakavyofaidika  na mapenzi hayo.
Mitazamo pia inawafanya watu kujiingiza katia hii biashara kwa kuwa wasichana wengi waliojiingiza katika maahusiano haya uona,mahusiano haya yana raha zaidi kushinda ya kushirki na mwanaume.kwa kuwa wameshaweka mitazamo hiyo huona kweli na kuendeleza misimamo yao ambayo inaendelea kuwapoteza wengine wana msemo wao ”wanaume pasua kichwa”   hivyo mahusiano hayo yana nafuu. 
Kwenye wengi kuna mengi na ukistaajabu ya Musa utayaona ya firauni, kuna wengine wanaofanya mahusiano haya ni fasheni na ndio kwenda na wakati na kujua utandawazi,wanaona sifa kuitwa au kuonekana wasagaji hasa watu maarufu kama wanamuziki na waigizaji.
Sawa tumelifumbia macho jambo hili na kufanya kama hatulioni hata tukiliona hashtuki na tukishtuka tunashtuka kidogo nakuacha maisha yaendelee,tunalionea aibu kulizungumza nakulijadili kwenye kadamnasi kwakuogopa kuonekana tunatetea au tunashabikia vitendo hivyo.
Lakini kiukweli imefika wakati tuongee na jamii na familia kueleza watoto wetu, dada zetu, mama zetu na rafiki zetu kwamba  kitendo hiki cha mahusiano ya jinsia moja yanaathari nyingi katika jamii na wanaojihusisha na mahusiano hayo.
Maradhi ni hatari moja kubwa iliyopo katika mahusiano ya jinsia moja, maradhi kama magonjwa ya zinaa (kaswende na,kisonono),mambukizi ya virusi vya UKIMWI na uwezekano wa kupata kansa ya shingo ya kizazi kutokana na mfumo mzima na vifaa wanavyotumia wakati wa kujamiiana ambavyo vina ruhusu  majimaji ya miili yao kukutana na hivyo kuwawekakatika hatari kama mmoja ameathirika”Maambukizi yapo ya magonjwa ya zinaa,UKIMWI na hata ri ya kupata kansa ya shingo ya kizazi kutokana na majimaji na vifaa” AlisemaDr. Merdad Paschal Nyalali  kutoka Haydom Lutheran Referal Hospital Manyara.
Pia wanawake wengi wanaojihusisha na biashara hii hujihusisha kimapenzi na watu wengine wanawake kwa wanaume hivyo kuwa katika mapenzi ya mtandao ambayo ni hatari kwa maambukizi ya magonjwa mbalimbali”Baaadhi ya watu naoshirikiana nao wana boifrendi(wapenzi )wao  nawengine ni wake za watu”. Anasema muathirika wa usagaji.
Matatizo ya kisaikolojia pia huwakumba wanawake wengi wanaoingia katika mahusiano haya ,japo wana sababu zao mbalimbali,za kujiingiza katika biashara hii lakini mioyoni mwao wanajua kwamba jambo hili si jema na halikubaliki kwenye jamii  kwahiyo huwa hawajiamini na huona kama wanaonewa(ndio maana mara nyingi watu wa namna hii huwa na maneno machafu na matusi).
 Wasagaji wale wanaosaga wenzao huwa wanajihisi niwanaume na huwa hawataki kuitwa au kufananishwa na wanawake,huvaa, hutembea na kuwa na tabia kama za kiume.
Mara nyingi wasagaji huwa ni watumiaji wazuri wa madawa ya kulevya na vileo ili kuweza kuhimili misongo waliyonayo”marafiki zangu hutumia vitu vikali ili kupata stimu unajua hii kazi saa zingine haiendi bila hivo vitu…mimi huwa na tumia pombe tu kawaida”.
Watu wenye mahusiano ya kimapenzi ya jinsia moja  wanapojulikana ni nadra sana kupata nafasi za kuajiriwa kwakuwa wanaonekana watofauti katika jamii na hamna mtu anaekubali kampuni au taasisi yake iwe na watu wa aina hiyo kwa kuwa hata eleweka katika jamii.
Kidini pia, dini zote hazikubaliani na vitendo hivi,hivyo mara nyingi kunatokea kutokuelewana kunapotokea kashfa kama hizi sehemu za ibada. Pia ni rahisi sana kwa watu wa aina hii kutengwa na kutokuruhusiwa kuingia nyumba za ibada kama misikitini na makanisani.
 Usagaji huchochea Mmomonyoko wa maadili kwa kuwa watu wengi  wanakua hawaheshimiani na kwavile mambo haya yanafanywa hadharani hadi watoto wadogo wanaonana kudharau na wengine na hivyo kuipelekea jamii kuwa ndivyo sivyo.
Mimi naamini kwa kushirikiana kwetu kama wananchi na wanajamii tunaweza kulishinda hili tatizo kwa kufanya na kuwajibika yafuatayo.
 Sheria zipewe meno zaidi na ztumike ipasavyo kudhibiti vitendo hivyo,kwasasa Tanzania inayo sheria inayokataza mahusiano ya jinsia moja “Sheria ya makosa ya jinai 2002 kifungu 157 inakataza mahusiano ya kimapenzi ya jinsia moja na adhabu yake ni miaka mitano” lakini sheria hii inaonekana kulegalega na watu waliowengi hawaijui na hivyo kutofanya kazi ipasavyo.
Hivyo basi kuna kila sababu ya kuanza kuzifwatilia hizi sheria nakuhakikisha zinafanya kazi ipasavyo nakuisaidia jamii na nchi yetu kwa ujumla.
Itolewe elimu ya kina kwa wasichana hawa kuwaeleza madhara ya biashara wanayofanya kiafya kwamba kuna uwezekano mkubwa  wa kupata magonjwa ya zinaa na ukimwi.Na waache kujidanganya kwamba hayo mapenzi ni salama.
Viongozi wa dini watusaidie katika hili kukumbusha waumini wao nini dini haitaki kuhusu mapenzi haya  ya jinsia moja. Elimu na mafunzo ya kidini pia yatolewe kwenye ngazi ya familia ili kuweka misingi imara na iliyo bora kwa watoto.kila mzazi hakikishe kwamba anamfundisha na kumtia hofu ya Mungu mtoto wake.
Wazazi wahakikishe wanapata muda wa  kufatilia mienendo ya watoto wao wanapokuwa,wanaposhinda,michezo wanayocheza na watu wanaoshi nda nao.Wawajengee uhuru na uwezo wa kusema na kueleza yale yanayowasibu (maana watoto wengi katika familia za sasa hivi hawana zile nafasi za kueleza matatizo na mambo yanayowasibu).Hivyo kukuta  watoto wanatendewa vitu visivyofaa lakini hawawezi kusema na wazazi wanapokuja kushtuka mtoto keshaharibika.
Maeneo hatarishi yafutwe na kuondelewa mfano zile sehemu maarufu  kama nyumba zawahaya (samahani lakini ndivyo zinavyoitwa) maeneo mbalimbali jijini Dar es salaam yaondolewe maana yanachochea na kufundisha watoto tabia zisizofaa.
Vilevile zitungwe sheria kulinda na kuongoza sehemu hizi za starehe,maana vitendo hivi vinafanyika na tunajua vinafanyika lakini sheria haiwabani wenye kumbi hizi,sasa sheria zikija na kuwabana hili tatizo litapungua na kuisha kabisa.
Jambo jingine litakaloweza kuweka mambo sawa katika tatizo hili ni kuwekwe mifumo mizuri ya kiuchumi itakayomwezesha mwanachi wa kada mbalimbali kuweza kupata fursa sawa ya kumiliki mali,na kuweza kukidhi mahitaji yake ya kilasiku na familia yake.
Nikinukuu maneno kutoka kwenye makala inayosema”USHOGA NI MATUNDA YA MIFUMO MIBAYA YA KIUCHUMI NA JAMII” ya  aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake(TAMWA) Bi Ananilea Nkya anasema”ushoga na usagaji ni moja ya matunda mabaya ya mfumo wa uchumi wa kibepari ambao kwa kawaida hutoa fursa kwa wachache wenye nguvu za kimadaraka na kifedha na kuwaacha wananchi wengi wakiwa wamechanganyikiwa kutokana na kukosa fursa ya kupata ujira na maisha endelevu”hivyo basi kuna haja ya kuurekebisha mfumo uliopo ili uweze kuwa mfumo wenye kutoa fursa kwa watu wote na hivyo kupunguza watu wakiwemo wasagaji kutafuta njia za mkato za maisha.
Kizuri zaidi huu mfumo utawezesha watu kutotumia muda mwingi kuzunguka katika kutafuta riziki kwa kuwa fursa zitakuwa za wote. Na hivyo kutumia muda mwingi na watoto na familia na kujua maendeleo yao  na mienendo yao kwa ujumla.
Tuzingatie na kufwata maadili yetu yaliyopo tufundishe jamii yetu kuhusu utandawazi katika mlengo chanya na si kama ilivyosasa ambapo kila mtu hadi watoto wanajifunza wenyewe na marafiki zao kuhusu mitandao na kompyuta. Na vyombo vya habari vizingatie maadili yaliyopo hata kama yapo kibiashara zaidi.
Na serikali kupitai mamlaka ya mawasiliano (TCRA) ingetafuta namna ya kudhibiti baadhi ya programu ambazo hazina manufaa kwa wananchi na taifa kwa ujumla (kama walivyo fanya China )
Hili ni tatizo, hatuna budi kulikubali na kulifanyia kazi kama wanajamii ifike mahali tulijadili hili swala kwa uwazi na ukweli na kutengeneza jamii isiyo na mahusiano ya kimapenzi ya aina hii.kwa maana ukweli tunaujua na hatuna budi kuukabili pia tatizo lipo hatuna budi kulitatua  maana wanasema dawa ya tatizo ni kulitatua si kuikimbia.

HII MAKALA NILIANDIKA NILIPOKUWA NAJIFUNZA KUANDIKA MAKALA